20 PERCENT "Kwanini Nifanyie Video Afrika KUSINI ?" Unknown "Kwanini Nifanyie Video Afrika KUSINI ?" - 20 PERCENT >>>>Msanii Wa Muziki wa Bongo Fleva, Abbasi Hamisi ‘20 Percent’, amesema hatofanya video nchini Afrika Kusini kama wafanyavyo wasanii wengine kwa kuwa kwa sasa video zake ni za uswahilini hazihitaji kufanyika nchini humo. Msanii huyo aliyewahi kunyakua tuzo 5 za Kili alisema licha ya kuwa na uwezo wa kufanya video za nyimbo zake nchini humo, lakini kwa sasa bado hana wimbo unaohitaji video kutoka huko. “Kwa sasa nina wimbo unaitwa ‘Mbaya hana Sababu’ ambao nitaufanyia hapa nchini na naamini video yake itakuwa bora na itafanya vizuri hata kama sitairekodia Afrika Kusini kama wafanyavyo wengine,” alisema 20 Percent. Mkali huyo mwenye nyimbo za hisia aliongeza kwamba muziki wake si wa kushindana na msanii mwingine yeyote ndio maana hana haraka katika utoaji wa nyimbo zake pamoja na muziki wake. “Mimi sishindani na mtu katika muziki wangu nafanya kama akili yangu inavyotaka na nyimbo zangu natoa ninapoona nipo tayari kutoa na si kushinikizwa na watu,” alieleza. A post shared by msetoea.com (@msetoea) on Mar 14, 2016 at 2:39am PDT TOA MAONI YAKO HAPA,MATUSI HAPANA Tweet Share Share Share Share DO NOT FORGET LIKE OUR PAGE BELOW TO GET MORE SONGS FOR RESPONSE